Matthew 22:41-45

41 aWakati Mafarisayo walikuwa wamekusanyika pamoja, Isa akawauliza, 42 b“Mnaonaje kuhusu Al-Masihi?
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
Yeye ni mwana wa nani?”

Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”

43Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho, anamwita Al-Masihi ‘Bwana’? Kwa maana asema,
44 d“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’

45Kama basi Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ awezaje kuwa mwanawe?”
Copyright information for SwhKC